Miaka ya
nyuma wazee wetu waliweza kulala kwenye nyumba za udongo na nyasi ambazo hazina
ulinzi kama ilivyo hivi leo, lakini zaidi ya kuamini pia walikuwa salama. Kuna watu
wachache waliomiliki magari, hawakuhofu kuibiwa maana usiku walipaki magari yao
nje ambako kulikuwa na usalama wa kutosha.
Leo tunaishi kwenye nyumba za matofali zilizo na madirisha
pia milango ya chuma zikiwa na uzio wa umeme pamoja na walinzi lakini bado
hatuko salama kabisa, kwanini?
Mathayo 24:12 “na kwasababu ya
kuongezeka kwa maasi, upendo wa wengi utapoa”
Mtu yeyote anayetenda dhambi, na kuizoea hatimaye inakuwa ni
sehemu ya maisha yake hivyo hawezi kuishi bila kuitenda. Katika maisha ya jamii
ya leo, kupokea rushwa imekuwa ni kitu cha kawaida, zaidi tunapoangalia maadili
ya jamii nzima yanavyopotoka wote tukiwa mashahidi jinsi ambavyo vijana
wanavyojihusisha katika mahusiano ya mapenzi mapema. Katika mengi ambayo
tunayaona ya kawaida na kuchukuliana nayo, ndivyo jinsi upendo katika jamii
unavyotoweka.
2 Timotheo 3:1 – 5
Kizazi cha leo tumekuwa na roho ya mimi kwanza, watu
tunajipenda zaidi wenyewe na kujijali kuliko wengine, na hakika ni nani kati
yetu asiyependa fedha? Siku zote fedha ndiyo chanzo au msingi wa maovu yote
maana aliye na pesa ndiye anayeheshimiwa akiweza pia hata kununua haki ya mtu
mwingine, na kwa namna hii kilemba cha kiburi kinakuwa juu ya kichwa chake.
Kutoka 20:12 “Waheshimu
baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na
Bwana, Mungu wako. Tofauti kabisa heshima na utii kwa wazazi wetu havipo kabisa
siku hizi, maana kama kijana anamahusiano ya kimapenzi na mtu anayeweza kumzaa
haiwezekani heshima kwa wazazi wake ikawepo? Zaidi kama tumejaribu kutafakari
siku hizi vijana ndio wanaokufa mapema zaidi kuliko watu wazima na wazee.
Kutokana na kuongezeka kwa uhalifu imekuwa ngumu sana kutoa msaada kwa
yoyote, hasa tunapojua kwamba unaweza kuwa mwema lakini malipo yakawa tofauti
kabisa, zaidi kukuumizwa na kurudishwa nyuma. Inasikitisha tunapofahamu ni
mahusiano mangapi mtu ameshakuwanayo kabla hajaoa, pale tu anapojua jinsi
inavyomuathiri katika maisha yake ya baadaye na ndoa yake kiasi kwamba ndoa
nyingi hazidumu.
Kazi na masumbufu ya maisha yamechukua sehemu kubwa sana ya
maisha yetu, hatuna muda wala kuona umuhimu wa kupendana na kujali tunapokuwa
hai au katika shida na ugonjwa, lakini kwenye msiba tunakusanyika na kuonyesha
masikitiko na huzuni. Kutokana na mizigo ya dhambi ukali umejengeka ndani yetu,
kwa jambo dogo tunawekeana chuki ya maisha na kulaani tukidhani kwamba pesa
ndilo jawabu la mambo yote.
Kama Yuda
alivyomsaliti Yesu, ni kutokana na vitu vya kupita tu zaidi anasa zinatupelekea
kusalitiana na kujenga chuki baina yetu. Ukifuatilia kwa karibu, jamii ya sasa
tunapenda sana anasa maana imekuwa ni sehemu ya maisha. Tumekuwa tukikimbiza
sana maisha kuliko ilivyo kawaida ili kupata kila kitu haraka haraka. Yeyote
anayepanda katika mwili atavuna uharibifu, lakini yule anayepanda katika roho
atavuna uzima wa milele.
Wynn Las Vegas & Encore - Jeopardy - JT Hub
ReplyDeleteJeopardy. 경기도 출장마사지 Jeopardy. 안동 출장마사지 Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. 청주 출장샵 Jeopardy. 광주 출장마사지 Jeopardy. Jeopardy. 대구광역 출장마사지 Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy. Jeopardy.