Ukiwa ni
mkazi wa mji ambao wanaishi watu toka sehemu za tofauti mwa taifa, ni rahisi
sana kumgundua mgeni anayetoka mkoa mwingine hasa kwa lafudhi yake pia lugha,
na zaidi sana mavazi.
Lakini picha nzuri unaipata ukitembelea au kama unaishi nchi
ya ugenini, maana kwanza unajiona mgeni eneo lile lakini pia inakuwa rahisi
sana kumgundua mgeni mwingine au mwenyeji pia kwani katika mataifa yote ya
dunia tunatofautiana sana katika mavazi, lugha pia lafundi hata kama lugha ni
ile ile lakini zaidi sana hata rangi.
Mathayo 3:1 – 2
Mtu ambaye hajatubu, hayuko katika utayari wa kuupokea
ufalme wa Mungu, maana hajatengeneza mazingira halisi ya kuishi katika ufalme
wa Mungu. Lakini pia hata ambaye ametubu inawezekana kabisa bado hajaupokea
ufalme wa Mungu ila ndio anaelekea.
Unapoomba uraia wa nchi nyingine kuna vitu vingi sana
wanavyokufanyia usaili kwavyo; kama nchi unayotoka, historia yako, elimu yako,
kazi yako na kipato, ukubwa wa familia yako pamoja na dhumuni lako katika nchi
hiyo. Na ni pale unapomudu vigezo vyote ndipo utakapoweza kupata uraia wa nchi
ile.
Mathayo 4:17
Bwana wetu, Yesu Kristo aliuleta ufalme wa Mungu hapa
duniani, ili tuupokee na kuishi tukiongozwa na Roho Mtakatifu. Yesu ndiye
mwanadamu pekee aliyeishi bila kutenda dhambi ingawa alijaribiwa hata zaidi ya
tunavyojaribiwa leo hii.
Unapoupokea
ufalme wa Mungu, kwako kuiba sio chaguo, wala kusema uongo si hatua ya
kuifikia, tamaa haiwi tena sehemu ya maisha yako, ulevi wala uasherati vinakuwa
si tena mvuto kwako zaidi kila kinachoitwa dhambi unakichukia sana maana
unafurahi na kufarijika daima unapoishi katika ufalme wa Mungu. Hakuna mtu
anayechukia nyumbani kwao, walipo ndugu na jamaa zake.
Raia wa nchi
masikini anapokwenda kwenye nchi tajiri akafanikiwa sana na kupata kibali cha
kuishi huko atafanya kila awezalo kuzishika na kutozivunja sheria za hiyo nchi
kwani amepata sehemu ya furaha, faraja na amani pia.
Mathayo 13:44
Inatupasa
tuutafute ufalme wa Mungu leo, maana inawezekana tumeokoka lakini bado
tunashindana sana na dhambi kila inapoitwa leo, hata inafika wakati tunakata
tamaa. Tufahamu kwamba kuokoka ni hatua ya msingi sana tuliyoifikia ila ili
kumpendeza Mungu inabidi tuwe watakatifu, na hatuwezi kuwa watakatifu bila
kuupokea ufalme Wake.
1 Peter 1:15 – 16
Mathayo 6:33 – 34
Tabia moja
ya ufalme ni kuwa na kiongozi (mfalme) ambaye anahakikisha kila mtu anapata
anachohitaji maana yeye ndiye anayemiliki wote na vyote. Sisi tunahangaikia
sana maisha maana bado tunaamini sisi ni mali yetu wenyewe. Kama ambavyo mimi
na wewe tunahudumia familia zetu je, si zaidi sana Baba yetu wa mbinguni?
No comments:
Post a Comment