Siku zote za
maisha yetu katika wokuvu tunakutana na upinzani mwingi sana kutoka kwa
Shetani, ambapo mara nyingi Shetani haji kwetu yeye kama yeye ila anatumia watu
wa karibu sana.
Yamkini tunafahamu kuwa kitu ambacho kinaweza kumuumiza sana
mtu ni kile ambacho anakipenda sana, au mtu anayempenda sana. Tunapofanyiwa
ubaya na ndugu au jamaa wa karibu inatuuma sana kwa sababu ya ule upendo
tulionao juu yao.
Yusufu alitupwa katika shimo, lakini haikutosha akauzwa
utumwani na ndugu zake wa baba mmoja, lakini hata Yusufu alipokuwa waziri mkuu
wa Misri, hakutaka kulipa kisasi na kuwatenda ndugu zake mabaya ila aliwatendea
yakiyo mema. Mwanzo 37: 23 – 28 | Mwanzo 45: 3 – 11
Inawezekana kazini kwako wafanyakazi wenzako hawakupendi au
bosi anakuchukia; cha msingi ni kutokutizama ubaya wanaokutendea, ila wewe
timiza wajibu wako fanya kila lililo jema siku zote. Kama ambavyo mvua hunyesha
kwa walio haki na wasio haki, Mathayo 5:
43 – 48 | Mathayo 5: 20
Daima mtu anapokutendea lililo baya anategemea uumie sana
ndani yako, lakini anapoona kuwa wewe hujalihesabu alilofanya kuwa baya wala
hujali na unasonga mbele tu na maisha ukifanya mema, inamuumiza yeye zaidi.
Lakini unapotendewa baya likakusumbua, ukajawa hasira na kunuia kulipa kisasi,
hapo unampa nafasi Shetani kukutawala na kukuangamiza. 1 Peter 3: 9 - 12 | Mhubiri
7:9
Lakini pia sisi tuliookoka tunaposemwa vibaya hata
wanapojaribu kutulaani kwetu inabidi iwe ni furaha maana maandiko yanasema
watalaani lakini Mungu atazigeuza kwetu kuwa Baraka. Zaburi 109:28
Sauli alinuwia sana kumuua Daudi, maana alifahamu kuwa si
muda Daudi atamnyang’anya ufalme wake, hivyo akaruhusu hasira ikae ndani yake
juu ya Daudi, lakini hata Daudi alipopata nafasi ya kumuua Sauli hakufanya
hivyo kwani ndani yake hakukuwa na kisasi. 1
Samweli 24: 4 – 7 | 1 Samweli 26: 7
– 12
Shedrack, Meshack and Abendnego walifungwa na kutupwa kwenye
tanuru lililochochewa moto mara saba zaidi kwakuwa walikataa kuiangukia na
kuisujudu sanamu aliyoisimamisha mfalme Nebukandneza, lakini katika imani yao
Mungu alikuwa pamoja nao. Hata mfalme alipowaita watoke kwenye moto
hawakuonyesha kisasi chochote dhidi ya mfalme Nebukandneza. Daniel 3: 26 – 29, Mungu anatukuzwa na
kuonekana ukuu wake pale tunapoushindwa ubaya kwa wema.
Aliyekuwa mwanzilishi wa kampuni ya Apple computers, Steve
Jobs ilitokea wakati akafukuzwa kazi kwenye kampuni aliyoianzisha yeye wenyewe,
lakini alisema ilikuwa vema sana kwani alijipanga na kuanza upya hata akarudi
tena kwenye hiyo kampuni baada ya miaka mingi na kuwa bosi mkuu.
Kwahiyo inawezekana
kabisa ndugu au yule unayemtegemea akakufanyia baya hata ukajuta na kutaka
kumlaani, ila tunachotakiwa kufanya ni kumshukuru Mungu, kutomuhesabia hatia na
kusonga mbele, kwani inawezekana hiyo ni njia anayoitumia Mungu kukufikisha
kwenye mazuri na mafanikio zaidi. 1 Thesalonike 5: 18
No comments:
Post a Comment