Sheria zote
alizoziweka Mungu wetu wa Mbinguni, ni mahususi ili kutulinda, zaidi sana ili
tukaishi kwa furaha na amani pia tufanikiwe.
Mwanzo 2:16 – 17
Katika kila jambo, na kabla hatujafanya lolote lile yatupasa
tukae chini na kutafakari kwanza, maana Mungu anasema hatuwezi neno lolote bila
Yeye kwani Yeye anaufahamu mwanzo wetu tokea mwisho.
Kumbukumbu la Torati 5:13 – 14
Mungu
amesema tufanye kazi siku sita, ya saba tupumzike akijua kabisa kwamba mwili
katika uasilia wake unahitaji kupumzika, ili uwe na afya njema na kuweza
kukabiliana na majukumu yanayofuata baada ya hapo.
Kinyume sana siku hizi tunafanya kazi mfululizo bila
kupumzika, tukitumia vinywaji hata dawa zakusababisha nishati ya ziada mwilini,
ndio maana watu wengi wana magonjwa ya moyo, kisukari, kansa na mengine mengi.
Kutoka 23:10 – 11
Ardhi inatakiwa ilimwe kwa miaka sita tu, na katika mwaka wa
saba tunatakiwa tuiache ipumzike ili irejeshe rutuba, lakini sisi tumetizama
njia mbadala ya kuweka kemikali tunazoziita mbolea ili uzalishaji uendelee siku
zote kwa wingi, hivyo tunaishi na matokeo ya kula vyakula visivyo na
virutubisho halisi kwa ajili ya miili yetu hata kupelekea maisha yetu kuwa
mafupi zaidi kutokana na magonjwa yanayosababishwa na kemikali hizi.
Neno la
Mungu linapotuambia usizini wala kumtamani mwanamke asiye mke wako, ni ili
kutuepusha na watoto wasiotarajiwa ambao wanaishia kuwa watoto wa mitaani ambao
hawakupata pia hawapati malezi sahihi ya baba na mama, zaidi ukishazini
unapoteza uthamani wako katika ubinadamu na taswira Mungu aliyotuumbia ndani
yetu.
1 Wakorintho 6:18 –
20
Hakuna ambaye anataka kati yetu mke wake au mume wake atamaniwe
na mtu mwingine, ambapo hili limekuwa tatizo sana katika maisha ya sasa hata
watu kufikia hatua ya kuuana.
Unapoiba,
unakuwa ni zaidi ya myonyaji kwani unachukua mali ambayo imetokana na jasho la
mwenzako bure kabisa, na kwa namna hii tumeshuhudia wezi pamoja na majambazi
wakichomwa moto na kuuliwa, maana hakuna anayekubali jasho lake liende bure awe
mtumwa siku zote akiwanufaisha wengine.
Waefeso 4:28
Kwanini
tumpende Mungu zaidi ya vyote na wote? Mungu ndiye muumba wetu, ndiye
aliyetukomboa pia toka mikononi mwa shetani, lakini zaidi anatupatia na
kututimizia mahitaji yetu ya kila siku hivyo Yeye tu ndiye anayepaswa kupewa
upendo wote na heshima.
Mark 12:29 – 30
Tusipowaheshimu wazazi wetu ambao tunawaona, haiwezekani kumheshimu na kumpenda Mungu ambaye hatumuoni.