Unapomwendea mwajiri wako katika hitaji lako, huwezi ukaenda tu nakumwambia hitaji lako bali inakupasa uende ukiwa umejipanaga vema kukabiliana na maswali atakayokuuliza. Vivyo hivyo, hata mzazi anapopelekewa hitaji na mwanaye, atahitaji kufahamu umuhimu pia ulazima wa yeye kutimiza lile hitaji.
Ndivyo
ilivyo hata kwa Baba yetu wa Mbinguni, ambaye siku zote anahitaji twende kwake
tukiwa na hoja zenye Nguvu, ili tupate kupewa hitaji letu.
Isaya 41:21
Katika
maisha yetu ya wokovu, inawezekana kabisa hatuendi katika utimilifu unaotakiwa
ndio maana hata tunapokuwa na mahitaji ya msingi ya kuyapeleka kwa Mungu
hatuwezi kupokea maana hatuna hoja za msingi hasa za kuzifungamanisha.
Hakuna mzazi ambaye anajua kabisa mtoto wake bado hajakua
vya kutosha akaanza kumkabidhi majukumu mazito au kumpa nyenzo zilizo nje ya
uwezo wake.
Hezekia
alipougua, hoja yake ya msingi mbele za Mungu ilikuwa kumkumbusha Mungu jinsi
ambavyo alikwenda mbele zake kwa ukamilifu wote, hata Mungu akakumbuka na
kumponya tena akamuongezea miaka kumi na tano ya kuishi.
Isaya 38:1 – 6
Wengi wetu inawezekana tumeshakutana na fulsa mbalimbali
wakati tunakua, ambazo pia huwa tunaziendeleza kwa watoto wetu. Mzazi
anapomwambia mwanaye akifaulu mtihani atamnunulia zawadi au kitu anachokipenda
sana, na ikawa mtoto akajitahidi na kufaulu mtihani basi mzazi anakuwa kwenye
msukumo mkubwa wa kutimiza ahadi yake. Zaidi sana kwa Mungu wetu, tunapoenenda
katika ukamilifu wote Naye atatimiza ahadi zake kwetu.
Isaya 43:26
Unakuwa na
ujasiri sana unapokwenda mahali kudai haki yako, hasa unajua kwamba hakika hiyo
ni haki yako, zaidi sana Mungu wetu anatupenda na kutujali kuliko hata wazazi
wetu wa hapa duniani.
Bwana Yesu
anasema kwamba tukimkiri Yeye mbele za mataifa, hakika naye atatukiri mbele za
Baba yake aliye mbinguni.
Mathayo 10:32 – 33
Kuna siri moja ya kumkiri Yesu mbele za watu siku zote.
Mungu anatutizama katika uhalisia kwamba sisi tumebeba taswira yake, hivyo
tunapomkiri mbele za watu kwa matendo na maneno yetu tunampa msukumo wa Yeye
kufanya kitu katika maisha yetu siku zote.
Hatasiku
moja huwezi kurudisha bidhaa feki kwenye kampuni halali, maana inapofika pale
wao hawaitambui kwasababu haiku kwenye nakala zao. Hivyo haiwezekani ukawa
unamkiri Yesu kwa mdomo tu bila matendo ukategemea ujenge hoja za hapa na pale
katika hitaji lako naye akupatie sawasawa na kuhitaji kwako.
Mathayo
7:22 – 23
Mtumishi Mungu akubariki kwa maneno yenye baraka na Nguvu ya Mungu.
ReplyDelete