Kuumizwa au kuumia ni hali ambayo ipo katika maisha yetu ya
kila siku, na kwa namna moja au nyingine huwa tunajikuta tumeumia, lakini
inatupasa kufahamu na kutambua kuwa mabaya yote huja kutoka kwa mwovu Ibilisi
na Shetani ambaye kamwe hataki kutuona salama.
Mara nyingi
tunapoumia tunashikwa na uchungu mwingi sana hasa aliyetuumiza anapokuwa ni
ndugu au jamaa wa karibu sana. Haizuiliki kuwa na uchungu lakini hatutakiwi
kuwa katika hali hiyo muda wote.
Zaburi 30:5b
Muhubiri 7:9
Inawezekana
kabisa tumeshindwa na kuanguka katika mambo mengi sana ingawa tulifanya yote
katika usahihi hata kujiuliza kama kweli Mungu yuko upande wetu? Baadhi yetu
tumewekeza sana kwenye biashara, pengine elimu au hata ndugu zetu lakini malipo
ni kinyume kabisa na jitihada. Yamkini hata tumepoteza ndugu wetu wa karibu
sana tuliowapenda, tunaweza hata kumuuliza Mungu kwanini? Sisi hatujui, wala
haina haja ya kuwa kwenye hali ya msongo wa mawazo ila ni kumuachia Mungu na
kusonga mbele tena kwa Imani.
Mithali 3:5
Zaburi 50:15
Kwa kujaribu
kutumia akili, maarifa au hekima ya kibnadamu ndipo wengi sana tumepotea, hata
ikafikia mahali tukajawa na hofu sana kiasi cha kupoteza maisha. Wangapi
tunajua kuwa wapo wengi waliowaza sana kwa uchungu hata kukatisha maisha yao
mapema?
Mithali 3:7 – 8
Kama
kungekuwa na watu wa kukata tamaa au kuishi kwenye uchungu pamoja na hasira
maishani mwao basi ingekuwa Yusufu na Daudi, kwani walipata shida sana lakini
Mungu aliacha yote haya akiwa na kusudi maalum katika maisha yao.
Isingekuwa
uvumilivu Yusufu angekata tamaa na kujutia maisha yake, lakini mbali na
kuvumilia kama angekuwa na uchungu pamoja na kisasi hakika angewarudi ndugu
zake walipokwenda Misri.
Lakini pia Daudi
angejawa na kisasi, hakika angemuua Sauli mara ya kwanza tu Mungu alipomuweka
mikononi mwake, hasa wenzake walipomsihi ammalize au awaruhusu wao wammalize,
lakini Daudi aliacha kusudi la Mungu litimie.
1 Samuel 24; 26
Siku zote,
Mungu akishaweka hitimisho hatupaswi kabisa kuendelea kujiuliza na kukaa kwenye
machungu na hasira kwakuwa kila siku ni mpya. Unapoishi na hasira au uchungu wa
jana, tayari umeiharibu jana, unaiharibu na leo pia hata kesho.
Kutoka 3:14
Kuna usemi
unasema “ Ni maamuzi yetu kuchagua
kuishi kwenye uhuru wa kusamehe au gereza la uchungu”.
No comments:
Post a Comment