Pages

Nataka Kuokoka Sasa Hivi!

Ndugu yangu, hakuna kilicho bora sana duniani na baada ya maisha haya zaidi ya roho yako? Je, unafahamu baada ya maisha ya hapa duniani kuna maisha mengine ambayo wewe una maamuzi ya asilimia mia kuchagua?
Fahamu kuwa kuna Mbingu na Jehanamu. Mshahara wa dhambi daima ni mauti, na mshahara wa mema ni uzima wa milele. Chagua uzima ukaishi milele kwakuwa maisha ya hapa duniani ni ya kitambo kifupi sana nayo yamejaa masumbuko na taabu nyingi sana kila inapoitwa leo.
Yesu anakupenda sana, inawezekana kuna mtu anakupenda sana ila Yesu anakupenda zaidi ya wote duniani hivyo nakushauri ukate shauri umfuate yeye maana atakupa kustarehe milele na kuurithi ufalme wa mbinguni pamoja naye.

Thursday, April 19, 2012

Kunuia Yaliyo Makuu



Ndoto ni kitu kizuri sana, hasa ndoto zenye kujenga na kutupa motisha. Wengi katika tulipokuwa wadogo tuliota maisha ya namna Fulani, ambayo ni mazuri sana yenye mafanikio bila kuwa na shida yoyote, lakini kuna usemi unasema ndoto huwa zinatimia walakini pia huwa hazitimii vile vile.

Kwanini huwa tunanuia au kupanga yaliyo makuu sana lakini inafikia wakati tunakata tamaa, hata kuona haiwezekani na kurudi nyuma? Tulipoupokea wokuvu tulikuwa na wito na moto wa hali ya juu sana katika kuitenda kazi ya Mungu, kusoma na kujifunza neno. Wengine tulinuia kuwa kama watumishi mbalimbali wakubwa duniani, lakini ile ari sasa imepotea, ule moto umefifia kama sio kuzima. Je, yale makuu tuliyonuia yameishia wapi?

Kunuia makuu ni jambo moja, na kufanikisha kile unachonuia ni chambo jingine tofauti kabisa kwani katika kufanikisha yale makuu tunayonuia siku zote lazima tulifuate na kulishika neno la Mungu linavyotuambia, vinginevyo hata tukitimiza nia zetu hazitakuwa za kudumu kwani hazina msingi wa kudumu.

Kuwatumikia wengine kunamuinua sana mtu siku zote, kama ambavyo Elisha alimtumikia Elia, hata akamwambia Elia kuwa si kwamba anataka tu kile alicho nacho ila anataka mara mbili zaidi ya roho iliyokuwa ndani ya yake. 2 Wafalme 2:9 – 14

Wenye uvumilivu siku zote katika Mungu hufika mbali sana hata kuona yale waliyonuia (ndoto zao) yakitimia kwa wakati ambao ni timilifu kwa Bwana Yesu, kama ambavyo Neno linasema kila kilicho kamili hutoka kwa Baba yetu wa Mianga. Yakobo 1:17

Tukimtizama Yusufu ambaye alikuwa akiota, lakini sio kwamba aliota tu ila aliamini na kuzishikilia ndoto zake hata zitimie, yamkini angekata tamaa mapema yote yasingewezekana kutimia, hata tunapotizama Yusufu aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa Misri akiwa na miaka 30. Mwanzo 41: 39 – 46

Kung’ang’ania kulimfanya Jakobo akashindana na malaika, hata akabarikiwa, lakini pia mara zote Eliyah alipomuambia Elisha asimfuate maana Mungu amemtuma sehemu nyingine, Elisha alikamjibu kama Mungu aishivyo na roho yako iishivyo sitakuacha kamwe. 2 Wafalme 2: 1 – 2

Usipokata tamaa unajiweka kwenye nafasi ya kumshawishi Mungu afanye kitu siku zote, maana Daudi katika magumu yote aliyopitia hakukata tamaa, ingawa aliwindwa sana na Sauli ili amuue lakini katika yote Daudi alimkabidhi Mungu. 1 Samweli 26:17 – 24

Mapenzi ya Mungu yatimie siku zote katika maisha yetu. Maana, kama tunampenda Yesu, tutampenda na Baba pia, hivyo hatutaishi tukitenda mapenzi yetu ila daima mapenzi ya Baba yatimizwe maishani mwetu. Tukijaribu kulazimisha mambo kwa namna yetu ya akili na maarifa hakika tutakuwa tunapingana na makusudi ya Mungu katika maisha yetu. Mungu anahitaji tumuombe, tujifunze neno lake siku zote na tujinyenyekeze kwake. Yakobo 4:10

No comments:

Post a Comment