Alama za tahadhari zipo na ziliweka ili kutulinda sote
kutokana na dhambi ili tusipate uharibifu wowote. Daima tunazungukwa na tahadhari nyingi sana katika maisha
yetu ili kuweza kuboresha zaidi wala si vinginevyo ingawa kama kawaida ya
mwanadamu yeyote huwa tunataka kujua kuwa nikifanya tofauti itakuwaje?
Mungu aliwatahadhalisha Adam na Eva kuhusu kutokula tunda la
mti wa ujuzi wa mema na mabaya lakini shetani alikuja akawadanganya nao wakala
na kuasi. Lutu, mkewe na binti zake wawili walipotolea Sodoma
walitahadhalishwa na malaika kuwa wasigeuke nyuma walakini mke wa Lutu aligeuka
nyuma. Nuhu aliwatahadhalisha watu wa nyakati zile kuwa gharika
inakuja waingie kwenye safina lakini wao walimuona yeye kachanganyikiwa.
Anayerudi nyuma ni sawa na mbwa kuyarudia matapishi yake au
nguruwe aliyeoshwa kurudia tena kujigaragaza kwenye uchafu. Uhalisia ni kwamba mwanadamu ana haiba ambayo haibadiliki
hasa kama hana Roho wa Mungu ndani yake, hata tunapotazama leo hii matatizo na
shida nyingi zinatukuta kwakuwa tunapuuza tahadhari zinazotuzunguka.
Kumbukumbu 27:15-26 Laana nyingi kutokana na kuasi kwa
heshima na utii. 1 Samwel 2:34 Laana inayomkumba Eli na nyumba yake baada ya
kumuasi Mungu. Neno la Mungu linasema wazi kwamba tunapokubali na kutii
tutakula mema ya nchi ila tukiasi tutaangamizwa kwa upanga, maana kinywa cha
Bwana kimenena haya.
Nyakati hizi imekuwa ni utaratibu vijana wadogo au mabinti
kukutana kimwili na watu wazima sana hata ndugu zao au jamaa wa karibu sana. Wizi, usaliti na kutokutii vimekuwa ni sehemu ya maisha
pengine hata msisitizo wa kufanikiwa.
Mathayo 24:12 Tamaa za sasa zinatupeleka kwenye maovu kuongezeka sana, ambapo hatima yake ni Mungu kukiteketeza kizazi hiki.
No comments:
Post a Comment