Mara zote; tunapotazama umbali tuliotoka ni rahisi sana kukata tama. Ni sawa na barabara inayoelekea mbali ambapo huoni mwisho wake.
Kutizama tulipotoka kunaweza kujenga kiburi/majivuno kama tuna mafanikio; lakini pia masikitiko/kukata tamaa kama tumehangaika sana bila kufanikiwa.
Tunapoomba na kusubiri majibu kutoka kwa Mungu kwa muda mrefu sana tunakata tamaa.
Ukishatizama umevuka na kuweza mangapi unakuwa na majivuno; zaidi pia ukifanikiwa sana unabweteka siku zote. LUKA 12:18-21
Mara nyingi Baraka za Mungu zinatupita kwakuwa tunakuwa makini kwenye mambo yanayotuteka akili pia manufaa yake ni ya kitambo sana cha hapa duniani; hasa mambo yaliyopita.
Amani haiji ila kwa upanga; Neno la Mungu ni zaidi ya upanga ukatao kuwili. WAEBRANIA 4:12-13
Yakobo hakuamini alipoambiwa mwanawe Yusufu yuko hai kwakuwa aliishi akitizama kitu uongo kwamba mwanawe aliraruliwa na myama mkali. MWANZO 45:25-28
Usiteswe na magumu yaliyopita, au wapi unakopita ila mtumaini Mungu pasipo kugeuka nyuma kama mke wa Lutu aliyegeuka nyuma na kuwa nguzo ya chumvi. MWANZO 19:23-26
Tujadiliane na kuelekezana njia sahihi ya kuurithi ufalme wa Mbinguni na uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu.
Pages
Nataka Kuokoka Sasa Hivi!
Ndugu yangu, hakuna kilicho bora sana duniani na baada ya maisha haya zaidi ya roho yako? Je, unafahamu baada ya maisha ya hapa duniani kuna maisha mengine ambayo wewe una maamuzi ya asilimia mia kuchagua?
Fahamu kuwa kuna Mbingu na Jehanamu. Mshahara wa dhambi daima ni mauti, na mshahara wa mema ni uzima wa milele. Chagua uzima ukaishi milele kwakuwa maisha ya hapa duniani ni ya kitambo kifupi sana nayo yamejaa masumbuko na taabu nyingi sana kila inapoitwa leo.
Yesu anakupenda sana, inawezekana kuna mtu anakupenda sana ila Yesu anakupenda zaidi ya wote duniani hivyo nakushauri ukate shauri umfuate yeye maana atakupa kustarehe milele na kuurithi ufalme wa mbinguni pamoja naye.

No comments:
Post a Comment