Heshima ni
kitu cha msingi sana katika maisha ya jamii, kiasi kwamba mahali penye heshima
panatawaliwa na upendo pamoja na Amani.
Jamii
tunayoishi imetawaliwa na dharau inayojengeka kutokana na mali, nafasi katika
nyadhifa fulani pia elimu ambapo ni tofauti kabisa na mpango wa Mungu, kwani
inatupasa kumheshimu kila mmoja haijalishi ni mkubwa au mdogo zaidi anacho au
hana.
1 Timotheo 5:1 – 2
Mara nyingi
tunakosa kubarikiwa kwa sababu ya jambo ambalo tunasema au kushabikia
tukimkosea heshima ndugu, jamaa, mzazi na hata mtumishi wa Mungu kwakuwa
tunaona yamkini kile alichokifanya si sahihi, ila jambo la msingi kukumbuka
siku zote ni kwamba ile nafasi aliyonayo mhusika sisi hatujamuweka ila Mungu,
na katika kumkosea heshima kwetu kitakachotupata ni laana.
Hesabu 12:1 – 14
Mambo mengi sana tunafanya au kusema tukiwakosea heshima
wengine kwa kuiga au kufuata mkumbo wa wengine au jamii inasemaje, lakini
tukumbuke kuwa katika mengi sana jamii huwa inakosea hivyo Neno la Mungu
inabidi likae kwa wingi ndani yetu na kutuongoza siku zote.
Kutoka 20:12
Haijalishi mzazi ana kasoro ya namna gani, au anafanya
makosa kiasi gani yamkini amekuwa mbaya kwako kwa mangapi lakini siku zote
tunatakiwa kumheshimu na kumshukuru Mungu kwa yote. Kuwa na mzazi bado ni bahati
sana maana wapo ambao hawana hata mmoja, zaidi tusipoweza kumheshimu mzazi
tunayemuona haiwezekani kumheshimu Mungu tusiyemuona.
Mara nyingi sana tumesikia na kushuhudia yamkini nasi
tumeshiriki kwa sehemu kuwasema vibaya viongozi wa ngazi fulani katika nchi
yetu ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini. Ikiwa kuna baya lolote au popote pale
ambapo wamekosema, sio jukumu letu sisi kuwahukumu na kuwakosoa kwa namna ya
kuwakosea heshima lah, ila siku zote hukumu ni juu ya Mungu kuwarekebisha yeye,
sisi yatupata kuheshimu tukiitii mamlaka.
Daniel 3:8 –
30
Ingawa Shedrack, Meshack and Abed-Nego walimwabudu Mungu wa
kweli, pia ilikuwa haki kwako
kutokuanguka na kuisujudia sanamu ya mfalme Nebuchadnezzer, hata hivyo
walitunza heshima yao juu ya mfalme kwa jinsi walivyomjibu kabla pia baada ya
kuingizwa kwenye tanuru la moto lilikokuwa limechochewa mara saba zaidi.
Tumuombe sana Mungu wetu atujengee roho ya heshima ndani
yetu, zaidi heshima ni kitu cha bure ambacho hakikugharimu unapokitoa zaidi
unapata akiba ya Baraka ambapo kwa wakati Mungu anakuinua. Wenye roho ya
heshima wanafika mbali sana katika maisha wakimuona Mungu akitenda mambo makuu
na kuwapigania sana.
No comments:
Post a Comment