Matatizo
mengi katika jamii yetu yanatokana na kila mmoja kujiinua, kutaka kutambulika
(umaarufu), pia kwasababu hatuna roho ya kujishusha.
Migogoro
mingi katika familia ni kwa kuwa kina mama wanataka kuwa nafasi sawa na kina
baba, wakijua kwamba wana uwezo wa kumudu majukumu, zaidi mpango wa haki sawa
kwa wote umebadilisha kabisa maadili katika jamii nzima.
Mwanzo 3:16
Matatizo mengi katika maeneo ya kazi pia yanatokana na
kutojishusha kwa mfanyakazi au mwajiriwa ambaye anaona anajua zaidi kuliko
mkubwa wake, ama ni haki yake. Nakumbuka wakati mmoja mama yangu aliniambia
kuwa “mwanangu mkubwa hakosei”, na si kwamba mama alimaanisha kuwa hakika
mkubwa hakosei ila yampasa mdogo kushuka.
Mwanzo 39:11 – 19
Yusufu alikuwa na kila sababu ya kujitetea na kupignia haki
yake, lakini aliamua kujishusha akiamini kwamba ndivyo inavyompasa kuenenda na
kufanya, na hakika alimuona Mungu akimpigania na kumuinua hata alipokuwa
gerezani.
Bwana wetu
Yesu alijishusha sana hata kufikia mauti ya msalaba. Ingawa Yeye ni mfalme wa
wafalme, lakini hakuishi katika jumba la kifaari, zaidi alipiga kambi na
wanafunzi wake popote. Lakini pia, hata alipokamatwa, akateswa sana na kutemewa
mate na kuishia msalabani, alisema “Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui
walitendalo”. Lakini, katika kujishusha kote huku ndipo tumepata wokovu mkuu na
ulio wa thamani sana leo hii.
Mathayo 8:20 | Luka 23:34
Yakobo 4:10
Mtu anayejishusha siku zote Mungu humuinua sana. Zaidi,
kujishusha ni kutohesabu vingapi tunapoteza ila kuachia kusudi la Mungu liweze
kutimia katika maisha yetu. Mwizi anapokuja kuiba hazina yako ambayo Mungu
alikusudia iwe yako, ataambulia kuchuma laana, lakini wewe utamuona Mungu
akikubariki kwa hazina zaidi.
Warumi 12:20
Unapomsaidia adui kwa moyo mkunjufu, unakuwa umejishusha kwa
kiasi kikubwa sana kwakuwa katika uhitaji wake kwa hali ya kawaida ndio wakati
mzuri wa kulipa kisasi. Tukikumbuka Daudi alivyojishusha kwa Sauli mara mbili
hata asimuue, na Mungu alimbariki na kumuinua Daudi.
Kujishusha
kunaghairi mabaya, hata kosa likasamehewa na kusahaulika. Abigaili
alivyojishusha na kumuokoa mumewe Nabali asiuliwe na Daudi, hata Daudi
akakubali ombi na kughairi uteketezaji aliokuwa amenuia nyumbani kwa Nabal.
1 Samweli 25:23 – 35
Kujishusha ni tabia ya Mungu ndani yetu, hivyo tunapojishusha
tunasababisha watu waione nuru ya Mungu ikiwaangazia, ndio maana mtume Paulo
alijishusha sana katika huduma yake. Kujishusha hakutizami tunapoteza mangapi
katika mwili bali tunaweka hazina kiasi gani Mbinguni kwa Baba yetu.
No comments:
Post a Comment