Pages

Nataka Kuokoka Sasa Hivi!

Ndugu yangu, hakuna kilicho bora sana duniani na baada ya maisha haya zaidi ya roho yako? Je, unafahamu baada ya maisha ya hapa duniani kuna maisha mengine ambayo wewe una maamuzi ya asilimia mia kuchagua?
Fahamu kuwa kuna Mbingu na Jehanamu. Mshahara wa dhambi daima ni mauti, na mshahara wa mema ni uzima wa milele. Chagua uzima ukaishi milele kwakuwa maisha ya hapa duniani ni ya kitambo kifupi sana nayo yamejaa masumbuko na taabu nyingi sana kila inapoitwa leo.
Yesu anakupenda sana, inawezekana kuna mtu anakupenda sana ila Yesu anakupenda zaidi ya wote duniani hivyo nakushauri ukate shauri umfuate yeye maana atakupa kustarehe milele na kuurithi ufalme wa mbinguni pamoja naye.

Tuesday, February 21, 2012

Kuushinda Ubaya Kwa Wema

Siku zote za maisha yetu katika wokuvu tunakutana na upinzani mwingi sana kutoka kwa Shetani, ambapo mara nyingi Shetani haji kwetu yeye kama yeye ila anatumia watu wa karibu sana.
Yamkini tunafahamu kuwa kitu ambacho kinaweza kumuumiza sana mtu ni kile ambacho anakipenda sana, au mtu anayempenda sana. Tunapofanyiwa ubaya na ndugu au jamaa wa karibu inatuuma sana kwa sababu ya ule upendo tulionao juu yao.

Yusufu alitupwa katika shimo, lakini haikutosha akauzwa utumwani na ndugu zake wa baba mmoja, lakini hata Yusufu alipokuwa waziri mkuu wa Misri, hakutaka kulipa kisasi na kuwatenda ndugu zake mabaya ila aliwatendea yakiyo mema. Mwanzo 37: 23 – 28 | Mwanzo 45: 3 – 11

Inawezekana kazini kwako wafanyakazi wenzako hawakupendi au bosi anakuchukia; cha msingi ni kutokutizama ubaya wanaokutendea, ila wewe timiza wajibu wako fanya kila lililo jema siku zote. Kama ambavyo mvua hunyesha kwa walio haki na wasio haki, Mathayo 5: 43 – 48 | Mathayo 5: 20

Daima mtu anapokutendea lililo baya anategemea uumie sana ndani yako, lakini anapoona kuwa wewe hujalihesabu alilofanya kuwa baya wala hujali na unasonga mbele tu na maisha ukifanya mema, inamuumiza yeye zaidi. Lakini unapotendewa baya likakusumbua, ukajawa hasira na kunuia kulipa kisasi, hapo unampa nafasi Shetani kukutawala na kukuangamiza. 1 Peter 3: 9 - 12 | Mhubiri 7:9

Lakini pia sisi tuliookoka tunaposemwa vibaya hata wanapojaribu kutulaani kwetu inabidi iwe ni furaha maana maandiko yanasema watalaani lakini Mungu atazigeuza kwetu kuwa Baraka. Zaburi 109:28

Sauli alinuwia sana kumuua Daudi, maana alifahamu kuwa si muda Daudi atamnyang’anya ufalme wake, hivyo akaruhusu hasira ikae ndani yake juu ya Daudi, lakini hata Daudi alipopata nafasi ya kumuua Sauli hakufanya hivyo kwani ndani yake hakukuwa na kisasi. 1 Samweli 24: 4 – 7 | 1 Samweli 26: 7 – 12

Shedrack, Meshack and Abendnego walifungwa na kutupwa kwenye tanuru lililochochewa moto mara saba zaidi kwakuwa walikataa kuiangukia na kuisujudu sanamu aliyoisimamisha mfalme Nebukandneza, lakini katika imani yao Mungu alikuwa pamoja nao. Hata mfalme alipowaita watoke kwenye moto hawakuonyesha kisasi chochote dhidi ya mfalme Nebukandneza. Daniel 3: 26 – 29, Mungu anatukuzwa na kuonekana ukuu wake pale tunapoushindwa ubaya kwa wema.

Aliyekuwa mwanzilishi wa kampuni ya Apple computers, Steve Jobs ilitokea wakati akafukuzwa kazi kwenye kampuni aliyoianzisha yeye wenyewe, lakini alisema ilikuwa vema sana kwani alijipanga na kuanza upya hata akarudi tena kwenye hiyo kampuni baada ya miaka mingi na kuwa bosi mkuu.

Kwahiyo inawezekana kabisa ndugu au yule unayemtegemea akakufanyia baya hata ukajuta na kutaka kumlaani, ila tunachotakiwa kufanya ni kumshukuru Mungu, kutomuhesabia hatia na kusonga mbele, kwani inawezekana hiyo ni njia anayoitumia Mungu kukufikisha kwenye mazuri na mafanikio zaidi. 1 Thesalonike 5: 18

Thursday, February 16, 2012

Proverbs 5

My son, pay attention to my wisdom;Lend your ear to my understanding,
That you may preserve discretion,And your lips may keep knowledge.

For the lips of an immoral woman drip honey,And her mouth is smoother than oil;
But in the end she is bitter as wormwood,Sharp as a two-edged sword.

Her feet go down to death,Her steps lay hold of hell.
Lest you ponder her path of life—Her ways are unstable;
You do not know them.
 
Therefore hear me now, my children,
And do not depart from the words of my mouth.

Remove your way far from her,And do not go near the door of her house,
Lest you give your honor to others,And your years to the cruel one;
Lest aliens be filled with your wealth,And your labors go to the house of a foreigner;
And you mourn at last,When your flesh and your body are consumed,
And say:
“How I have hated instruction,And my heart despised correction!

I have not obeyed the voice of my teachers,Nor inclined my ear to those who instructed me!
I was on the verge of total ruin,In the midst of the assembly and congregation.”

Drink water from your own cistern,And running water from your own well.
Should your fountains be dispersed abroad,Streams of water in the streets?

Let them be only your own,And not for strangers with you.
Let your fountain be blessed,And rejoice with the wife of your youth.
As a loving deer and a graceful doe,Let her breasts satisfy you at all times;
And always be enraptured with her love.

For why should you, my son, be enraptured by an immoral woman,
And be embraced in the arms of a seductress?
For the ways of man are before the eyes of the Lord,
And He ponders all his paths.

His own iniquities entrap the wicked man,And he is caught in the cords of his sin.
He shall die for lack of instruction,And in the greatness of his folly he shall go astray.

Tuesday, February 14, 2012

Uvumilivu Ndani ya Yesu


Mathayo 24:13 yeye atakayevumia hata mwisho, huyo ataokoka.

Maisha ya wokovu ni tamaduni pia desturi ya kujikana sana; na kutokana na kujikana huko unakuja uvumilivu. Mathayo 16:24

Kutokana na uhalisia huo ndio maana safari ya wokovu inakuwa ngumu sana hasa tunapokuwa katika hali ya mwili huu, kwakuwa mwili una kila hisia na mahitaji. Tunapotizama wenzetu wakifanikiwa na kuishi kwa furaha kutokana na njia zao potofu nasi tunajitahidi bila mafanikio inakatisha sana tamaa; lakini inahitaji sana imani na uvumilivu wa ziada kuweza kusonga mbele.
Yakobo 4:4 …rafiki wa ulimwengu ni adui wa Mungu.

Wengi wetu mara tu baada ya kuokoka tulikutana na majaribu tofauti kama kukataliwa na wazazi, marafiki kututenga, kutokubalika tena kazini hata jamii nzima. Kipimo cha imani ni pale unapokuwa huna kitu, huna msaada wala huna yeyote ila Yesu tu. Yohana 16:33

Mitume wasingekuwa na uvumilivu sisi leo hii tusingekuwa tunasoma habari njema za ufalme wa Mungu, lakini kutokana na uvumilivu wao ulio mkuu hata leo tunayo neema ya biblia; lakini zaidi ya yote endapo Bwana Yesu asingevumilia mateso hata kufia msalabani leo sisi tungekuwa wapi?

Siku zote inabidi tumuombe Mungu sana kuweza kushinda vishawishi pia majaribu ya adui zetu watatu; ambao ni MWILI | ULIMWENGU | SHETANI. Bila kuweza kuvumilia na kushinda tamaa za mwili, ulimwengu na majaribu ya Shetani hakika tutaishia kwenye moto wa milele.

Mhubiri Billy Graham alisema endapo kuna watu ambao leo Mungu anaweza kuwarudisha wakaishi akiamini watashinda yote ni Ayubu ambaye alimshinda Shetani, Nuhu aliyeushinda ulimwengu na Daniel aliyeushinda mwili.

Inakuwaje unamkana Yesu kwa mlo mmoja, pengine kwa kazi ya kitambo kifupi, au kwa nyumba nzuri yenye thamani nzuri za kupendeza, au kwa ajili ya mwanamke au mwanaume unayempenda sana; yamkini kwa ajili ya mtoto wako au mwili wako? Mathayo 10:37 – 38 | Mhubiri 3:20 | 1 Timotheo 6:10

Katika yote ni ubatili mtupu hapa duniani, hivyo inatupasa kuvumilia daima na kusonga mbele bila kukata tamaa.

Baba mmoja na mtoto wake (John) walikwenda safari ya mbali kwa gari, hata walipokuwa wakisafiri wakienda na kuuacha mji kabisa wakaingia kwenye nyika na kuzimaliza hata kufika kwenye jangwa ambapo kwa Bahati mbaya gari lao likatitia kwenye mchanga. Jitihada za kuitoa hazikuzaa matunda kwani kadri walivyojaribu ndivyo ikazidi kutitia. Baba akamwambia mwanaye kuwa inabidi atembee kurudi mjini kutafuta msaada ambapo itamchukua siku moja au zaidi hivyo yeye inabidi abaki kumsubiri pale. John akamtizama baba yake akienda na kutokomea kabisa hata giza likaingia, lakini kila alipokuwa akiwaza alikumbuka kuwa baba amesema anakwenda kutafuta msaada na atarudi kunichukua.

Basi wapendwa tusikate tamaa, tuwe na uvumilivu maana Yeye ajaye hatakawia maana kwa wakati wake atakuja kutuchukua.  Yohana 14:1 – 4

Monday, February 13, 2012

A Prayer of All Times


Dear my Father in Heaven,

Hallowed be Your mighty Name for Your mercy endures forever.
Give me strength to overcome all evil; and keep me from temptation thus I shall walk in Your path.
Let me sing Your name and give You glory day and night for there is none like You.
Lead me to Your way of salvation, and keep me there to the time I die.
Keep me from all the earthly ways but I shall only look at the cross of salvation.
Down deep in my heart I should not forget You since Your word is hidden in there.
If only I could have a wish, then it should be to seek You with all my heart.
Inherit in me and my descendant patience, love, peace and knowledge.
In Jesus name who is Christ and Lord, I pray!

Amen

Wednesday, February 8, 2012

Usikate Tamaa


Tunakata tamaa siku zote baada ya kuona yote tuliyojaribu yameshindikana, pia hakuna anayewezakutusaidia ama uwezo wa kila mmoja kando yetu umefikia kikomo; hapo sasa tunakubali matokeo kwamba tumefika mwisho na tumeshindwa.

Haiba moja kwetu siku zote ni kuyatizama mambo katika ugumu wake wala si katika urahisi wake, hivyo kinachotujia akilini ni kwamba haiwezekani wala haitawezekana.

Mwanzo 37 – 41, Yusufu ni kati ya watu waliokatishwa tamaa sana ikiwa ni pamoja na ndugu zake; baba yake alimkemea kuhusu ndoto zake, ndugu zake wakamuuza, Potifa akamuweka gerezani, Mnyweshaji alimsahau alipotolewa gerezani lakini kutokukata kwake tamaa kulimuinua juu ya wote. Kumbuka unaweza kumuangamiza muota ndoto lakini sio ndoto ya Mungu.

1 Samweli 17: 33, Daudi hakuhofia uzoefu wala ukubwa wa Goliati kwenye vita lakini alimuamini Mungu muweza yote. Daudi pia aliishi kwa muda mrefu mafichoni akikimbia kuuawa na Sauli, lakini hakukata tamaa kwamba ufalme alioahidiwa sio wake tena, ila aliamini kwa wakati Mungu atamuweka anapostahili. 1 Samweli 19: -

Samsoni alilaghaiwa na Delila, akakamatwa na kupofuliwa macho kisha akawekwa gerezani akisaga ngano. Lakini mwishoni walipomtoa kwenye ukumbi wa maonyesho ili awafanyie michezo, pale akasimama akishikilia nguzo mbili kuu za ukumbi, akamuomba Mungu amrejeshee nguvu zake walau mara moja alipe kisasi, maana aliamini inawezekana kwakuwa hakukata tamaa. Waamuzi 16:26 - 30

Mara nyingi tunakuwa kwenye mazingira magumu sana, masomoni, kazini hata nyumbani tukiona mambo hayaendi, kila tunachojaribu hakifanikiwi wala hakuna anayetuunga mkono, ila leo Mungu ana jambo nawe kuwa usikate tamaa kamwe maana ahadi zake ni za kweli tena za milele.

Inawezekana una kilema; umeokoka ila bado tamaa imekushika, bado unasema uongo, hujaacha udokozi, usengenyaji, pengine unaonjaonja pombe au sigara na pengine umejihalalishia mke wa pembeni ingawa siku zote inakuuma sana, na unataka kuacha ila shetani bado kakukamata kwenye kilema chako. Cha msingi ndugu yangu usikate tamaa, endelea kuomba kwa bidii na kufunga wala usimsikilize shetani akuhubirie maana yeye ni baba wa uongo, na zaidi ya yote ni mshitaki wetu daima.

Mark 10:27, Kwa Mungu yote yanawezekana, Pia kila jambo linawezekana kwake yeye aaminiye.
Ukitereza usikubali kubaki chini, na ukianguka inuka haraka usonge mbele wala usiangalie watu wanasemaje juu yako au wanakutizama vipi bali wewe mtizame Mungu ndiye anayetuwezesha katika yote. 

Naamini Mungu anapendezwa na watu wasiokata tamaa, maana anapoona shetani akikujaribu hata zaidi ya mara elfu moja nawe unasimama tu na kusonga mbele ama kwa hakika ataingilia kati, lakini ukishasema siwezi tena unakuwa umempa shetani ushindi usio wa lazima. Inawezekana pia kwa kuangalia umbali tukiotoka tunakata tama kabisa, lakini kwakuwa Bwana Yesu alishinda, nasi tutashinda na zaidi ya kushinda. Yohana 16:33

Tuesday, February 7, 2012

Alama Za Hatari


Alama za tahadhari zipo na ziliweka ili kutulinda sote kutokana na dhambi ili tusipate uharibifu wowote. Daima tunazungukwa na tahadhari nyingi sana katika maisha yetu ili kuweza kuboresha zaidi wala si vinginevyo ingawa kama kawaida ya mwanadamu yeyote huwa tunataka kujua kuwa nikifanya tofauti itakuwaje?

Mungu aliwatahadhalisha Adam na Eva kuhusu kutokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya lakini shetani alikuja akawadanganya nao wakala na kuasi. Lutu, mkewe na binti zake wawili walipotolea Sodoma walitahadhalishwa na malaika kuwa wasigeuke nyuma walakini mke wa Lutu aligeuka nyuma. Nuhu aliwatahadhalisha watu wa nyakati zile kuwa gharika inakuja waingie kwenye safina lakini wao walimuona yeye kachanganyikiwa.

Anayerudi nyuma ni sawa na mbwa kuyarudia matapishi yake au nguruwe aliyeoshwa kurudia tena kujigaragaza kwenye uchafu. Uhalisia ni kwamba mwanadamu ana haiba ambayo haibadiliki hasa kama hana Roho wa Mungu ndani yake, hata tunapotazama leo hii matatizo na shida nyingi zinatukuta kwakuwa tunapuuza tahadhari zinazotuzunguka.

Kumbukumbu 27:15-26 Laana nyingi kutokana na kuasi kwa heshima na utii. 1 Samwel 2:34 Laana inayomkumba Eli na nyumba yake baada ya kumuasi Mungu. Neno la Mungu linasema wazi kwamba tunapokubali na kutii tutakula mema ya nchi ila tukiasi tutaangamizwa kwa upanga, maana kinywa cha Bwana kimenena haya.

Nyakati hizi imekuwa ni utaratibu vijana wadogo au mabinti kukutana kimwili na watu wazima sana hata ndugu zao au jamaa wa karibu sana. Wizi, usaliti na kutokutii vimekuwa ni sehemu ya maisha pengine hata msisitizo wa kufanikiwa.

Mathayo 24:12 Tamaa za sasa zinatupeleka kwenye maovu kuongezeka sana, ambapo hatima yake ni Mungu kukiteketeza kizazi hiki.