Nchi zilizoendelea, kuna matajiri wenye magonjwa ambayo bado
madaktari hawajapata tiba wala suluhisho lake hivyo wanalipa pesa nyingi sana ili
kugandisha miili yao, hivyo warudishwe kwenye uhai pale tiba itakapopatikana ili
waweze kuishi muda mrefu zaidi.
Miaka ya nyuma, iliwezekana kulala bila kufunga milango kwa
makomeo, pia watu walipaki magari yao nje bila kuyafunga hata ilipofika asubuhi
hakukuwa na wizi wowote, lakini maisha ya leo tunafunga milango nyuma ya
milango ya chuma na kuweka ulinzi wote, pamoja na uzio wa umeme lakini bado
hatuko salama.
Mithali 14:12
Siku zote suluhisho la mwanadamu katika tatizo moja, kama
hajaongozwa na Mungu hakika linatengeneza tatizo jingine kubwa zaidi hapo
baadaye. Magari yanaturahisishia sana usafiri kila siku lakini pia ndicho
chombo kinachosababisha ajali mbaya kila siku. Pombe ilitengenezwa kama sehemu
ya starehe lakini ndio chanzo cha magonjwa sugu yasiyo na tiba hata sasa. Simu
za mkononi zinaturahisishia sana kuwasiliana lakini ndio chanzo cha maovu mengi
na ndoa kuvunjika.
Mithali 3:5 – 6
Mungu hakika
ndiye muweza wa yote, yeye anaifahamu mipaka ya dunia, Yeye ndiye anayesimamisha
falme na kuziangusha, Yeye ndiye anayetoa kibali kwa kila jambo, pia ni Yeye
anayeijua sekunde inayofuata hata kesho na milele yote, Yeye anajua milele ina
umbali wa kiasi gani, Yeye anauona mwanzo kutokea mwisho, Yeye anatujua kabla
hata mimba hazijatungwa kwenye matumbo ya mama zetu, Yeye ni yule yule milele
yote habadiriki. Unapojaribu kufanya mambo kwa ufahamu na njia zako hakika wewe
umepotea.
1 wakorintho 1:25
Watafiti
wanavumbua mambo mengi sana yanayoonekana mazuri, watu wanapata utajiri
kutokana na jitihada zao katika maisha na mafanikio pia yanaonekana lakini kama
sio mpango wa Mungu katika yote daima huwa ni ubatili tu, sawa na kujilisha
upepo chini ya jua.
Solomon
katika fahari yake alikuwa tajiri sana, alikuwa na mali kuliko mwanadamu yeyote
aliyewahi kuishi, alioa wake 700 na akawa na Masuria 300 lakini mwisho
alifahamu kuwa yote ni ubatili mtupu.
1 Wafalme 11:3 | Mhubiri 1:1 – 10
Jibu la
Ukimwi analo Mungu, Jibu la kuvunjika kwa ndoa analo Mungu, Jibu la ugonjwa wa
Kisukari, Kansa na Shinikizo la damu pia analo Mungu, Jibu la kuyumba kwa
uchumi analo Mungu, Jibu la kuongezeka kwa maasi na vita analo Mungu, Jibu la
utoaji mimba pia hakika ni Mungu pekee aliyenalo.
Ufunuo 3:17 – 19
Ukimtumainia mwanadamu leo atakusaidia bali kesho atakukimbia, yamkini atakushauri lililo jema leo lakini yawezekana kesho atakupotosha, maana binadamu tunabadirika ndio maana amelaaniwa mtu yule amtumainiaye mwanadamu. Lakini Mungu tu ndiye habadiriki, Naye atakupa jibu sahihi.
No comments:
Post a Comment