Ukubali na utiifu wetu kwenye sheria, amri na Neno la Mungu
ni muhimu sana katika maisha yetu ya wokovu, na zaidi sana ili kuweza kusonga
mbele tukimuona Mungu akitujenga upya na kufanya yaliyo makuu sana kupitia
sisi.
Katika hali ya kawaida sana kwa kila binadamu, inakuwa
rahisi sana kutii ila si kukubali, maana unatii ile mamlaka kutokana na hofu
hivyo ukatekeleza ila ndani yako hujakubaliana na hilo jambo. Lakini kukubali
kunakuwepo kutokana na Imani ndani yako, hasa Imani iliyo timilifu.
Isaya 1:19 Ukikubali na kutii utakula
mema ya nchi….
Sheria ya
Mungu ni nzuri sana kwani ipo ili kutulinda pamoja na kutuepusha na mabaya siku
zote za maisha yetu. Mungu alipowaambia Adam na Eva wasile tunda la mti wa
ujuzi wa mema na mabaya alitaka kuthibitisha kwamba wanamtii, lakini zaidi ya
yote endapo wamekubaliana na kile anachokisema.
Mwanzo 2:16 – 17
Viumbe wanaoishi kwenye maji wamekubali na wanatii sheria waliowekewa na Mungu, pia
ndege wa angani hata wadudu na wanyama wa porini, ndio maana siku zote wanaishi
bila shida. Lakini sisi binadamu ambao tuliumbwa kwa kwa mfano wa Mungu siku
zote tunajaribu kuhakiki uhalisia wa kile ambacho Mungu amekisema.
Mathayo 6:31 – 34
Matatizo mengi katika maisha siku hizi ni kwasababu kila mtu
anataka kuwa yeye na mahitaji yake, au kile ambacho yeye hasa anataka kukifanya.
Ni kutokana na mahangaiko pamoja na msongo wa mawazo katika kizazi hiki
tunaongezeko kubwa sana la magonjwa ya kansa, shinikizo la damu na kisukari.
Hii ni kwakuwa hatutaki kutii na kukubaliana na ukweli kwamba kesho tumuachie
Mungu, lakini pia ni jukumu letu kuutafuta ufalme wake kwanza na haki yake.
Bila Imani
inakuwa ngumu sana kukubali, kwani pale unapomuamini mtu ndipo unapoweza
kukubaliana naye. Usipomwamini mwajiri wako huwezi kuendelea kumtumikia, zaidi
usipomuamini mwenzi wako inakuwa ni ngumu kuishi naye pamoja.
Panapokosekana Imani kunajengeka mashaka na woga ambao
hutoka kwa Shetani. Ili kumuona Mungu katika uhalisia wake maishani mwetu
lazima tuwe na Imani timilifu maana haiwezekani kumpendeza Yeye pasipo Imani.
2 Timotheo 2:11 – 13
Mtu mwenye
utii na kukubali siku zote hubarikiwa, na katika mambo yake siku zote
atafanikiwa na kuwa juu ya mataifa.
Kumbukumbu la Torati 28:1 - 14
No comments:
Post a Comment