Mtu ambaye hali vyakula vyenye kuleta afya na kuulinda mwili
ikiwa ni pamoja na kunywa maji kwa wingi hakika hatakuwa mwenye afya nzuri, na
mara nyingi mtu huyu atasumbuliwa na magonjwa ya hapa na pale; ndio maana
ukiungua daktari anasisitiza sana upate chakula bora pamoja na maji ya kutosha.
Wengi wetu
tuko makini sana kuujali mwili, katika kuulisha chakula pamoja na tamaa zake,
lakini tunasahau kuwa mwili ni mavumbi, na hakika mavumbini utarudi tu. Sote
tunakula mara tatu kwa siku hasa kwa wengi wetu wenye maisha ya kawaida.
Mwanzo 3:19
Inatupasa
kufahamu kuwa mtu wetu wa ndani (Roho) nayo pia inabidi kula na kushiba kila
siku tena hata kula muda wote kwani mwili huu wa nyama hauishi milele ila roho
ndiyo itakayoishi milele. Roho zetu zinahitaji kulishwa chakula sahihi ambacho
ni Neno la Mungu. Kama ilivyo kawaida kuwa kile anachopanda mtu hakika ndicho
anachovuna, kwani huwezi kupanda mahindi ukavuna karanga.
Wagalatia 6:7
Wengi
tunapenda sana kusikiliza miziki, au kushiriki mazungumzo ambayo hayatujengi wala kutusaidia
kabisa, na pia nyakati tofauti tumekuwa tukitizama vipindi kwenye luninga
ambavyo vinatujaza uovu, zaidi pia kuna magazeti mengi ambayo sisi tunaoifuata
kweli hatutakiwi kujihusisha nayo kwakuwa yamkini usione ubaya wake sasa ila
kadri muda unavyosonga ile mbegu iliyopandwa inakua na kuanza kuzaa matunda.
Mithali 15:14
Inatupasa
tufahamu, unaposikiliza wimbo unaoelezea mtu na mwenzi wake wa zamani kwa muda,
kitakachokuijia akilini ni mwezi wako wa zamani pia. Hizi tamthilia
zinazoonyesha jinsi watu wasivyo waaminifu katika maisha na ndoa zao,
zinapoujaza moyo wako kwa muda hakika kitakachokutokea ni wewe kukubaliana
kwamba hiyo ndiyo hali ya maisha ya kuiendea na kuishi. Ukiishi kwa kusoma,
kuangalia na kusikiliza mizaha hakika nawe unatakuwa na mizaha tu.
Mithali 23:7a
Katika
maisha haya ya utandawazi, ambayo kila mtu ana uhuru wa kufanya chochote kile
anachoona kinafaa, hata wazazi wanakosa haki ya kuwakemea watoto wao; inatupasa
kukaa na kung’ang’ania katika sharia ya Mungu siku zote na muda wote. Si vema
kupoteza wokovu wako wa thamani sana uliopewa bure kwa ajili ya gazeti la
udaku, au tamthilia inayopita au mziki ambao unakuvutia sana kila
unapousikiliza.
Wagalatia 6:8
Zaburi 119:37
Kama Daudi alivyoamua kutokujizuia kumtizama mke wa Uria alipokuwa akioga, hata ikampelekea kutenda dhambi moja baada ya nyingine; inawezekana kabisa sinema tunazozipenda, magazeti au miziki ikatupelekea kutenda dhambi mbele za Mungu. Tutambue leo na kumuomba Mungu atusaidie, zaidi tuwe watu wa kujizuia sana.
No comments:
Post a Comment