Pages

Nataka Kuokoka Sasa Hivi!

Ndugu yangu, hakuna kilicho bora sana duniani na baada ya maisha haya zaidi ya roho yako? Je, unafahamu baada ya maisha ya hapa duniani kuna maisha mengine ambayo wewe una maamuzi ya asilimia mia kuchagua?
Fahamu kuwa kuna Mbingu na Jehanamu. Mshahara wa dhambi daima ni mauti, na mshahara wa mema ni uzima wa milele. Chagua uzima ukaishi milele kwakuwa maisha ya hapa duniani ni ya kitambo kifupi sana nayo yamejaa masumbuko na taabu nyingi sana kila inapoitwa leo.
Yesu anakupenda sana, inawezekana kuna mtu anakupenda sana ila Yesu anakupenda zaidi ya wote duniani hivyo nakushauri ukate shauri umfuate yeye maana atakupa kustarehe milele na kuurithi ufalme wa mbinguni pamoja naye.

Monday, August 1, 2011

Usigeuke Nyuma na Kumuacha Yesu






Mke wa Lutu aligeuka hakuweza kuvumilia wala kuamini kwamba yale yote waliyoyaacha Sodoma yalikuwa yakiteketea, pia inawezekana kabisa alikwenda mwendo mrefu akijishauri kugeuka atazame au lah, lakini mwishoni akakata shauri na kuamua kugeuka nyuma.
Ama kwa hakika neno la Mungu ni kweli tena lazima litimie, na kwakuwa alikiuka agizo walilopewa na malaika, mara tu baada ya kugeuka nyuma alibadirika na kuwa nguzo ya chumvi, na hapo ndipo mwisho wake ulipokuwa.
Shetani daima ni mshawishi ambaye hawezi kukushawishi mema hata siku moja, kwakuwa yeye huja kuua na kuharibu ila Yesu alikuja ili tuwe na uzima tena tuwe nao tele. Mke wa Lutu alitamani tena yale ya Sodoma, yawezekana alikumbuka jamaa zake, au mali zao zote walizokuwanazo, lakini sawa sawa na neno la Mungu kwamba rafiki wa dunia hawezi kumpendeza yeye hata siku moja.
Bwana Yesu anatuasa kuachana na vyote kisha tujitwike msalaba wetu na kumfuata maana vyote vya duniani vinapita tu kwakuwa tulizaliwa uchi tukiwa hatuna chochote pia tutaondoka tukiwa hatuna chochote. Huu ni uhalisia ambao shetani ametuficha wengi sana tunaohangaika na dunia hii na kumsahau Mungu wetu anayetuambia tuutafute ufalme wake kwanza na haki yake kisha yote tutazidishiwa maana fedha na dhahabu vote ni mali yake Bwana wa Majeshi.

No comments:

Post a Comment