Ni vema
kuchukua muda, na kujiuliza nia hasa za moyoni mwetu kumfuata Yesu maana
inawezekana tukaamini kuwa tunamfuata Yesu kumbe tunaifuata njia yetu wenyewe
bila kujua.
Je, tunaushikilia wokovu kwakuwa tunajua kuna hukumu
inakuja, au kwakuuogopa moto wa milele? Haya yasingekuwepo tungeendelea
kuupigania wokuvu na kuushikilia kwa lolote hata kufa?
Wengi wetu
ambao tumefikia na watakaofikia maamuzi ya kuoa, tunasukumwa zaidi na tamaa
zetu za mwili lakini si kwamba tuna upendo halisi ambao Mungu anataka tuwe nao;
maana kuna ndoa nyingi sana ambazo zina migogoro au kuvunjika kabisa kwakuwa tu
ule mvuto wa kimwili kwa mmoja au wote umepotea kabisa.
Mfanyakazi siku zote anaonekana mzuri sana hata akapewa sifa
nyingi na kupendwa pale tu ambapo hakosei, lakini siku akikosea haijalishi kuna
mangapi mazuri ameshafanya ila kama ilivyo haiba yetu binadamu tunasahau yote
mazuri na kutizama kosa moja.
Yohana 14:15 Yesu anasema tukimpenda
Yeye tutazishika amri zake.
Kuzishika amri zake ni kutekeleza tukitenda yale yote
aliyotuagiza, haijalishi kwamba tunaonekanaje katika jamii bali tuonekane wenye
haki kwake. Pia, haijalishi kuna mangapi tumekosa ila yatupasa kuing’ang’ania iliyo
kweli yake.
Daniel 3:17 – 18
Shedrack, Meshack and Abed-Nego walimwambia mfalme
Nebukadnezzer kuwa Mungu wao wanayemwamini atawaokoa na moto wa tanuru, lakini
hata isipokuwa hivyo hawawezi kuanguka na kuisujudu sanamu aliyoisimamisha
mfalme, maana walikuwa na uhakika na Mungu wa kweli ambaye wanamwamini na
kumtumaini.
Inawezekana
wengi wetu tupo katika wokuvu kwakuwa Mungu anaonekana jinsi anavyotubariki,
zaidi sana hatujapungukiwa kwa sasa, lakini ikitokea tumepungukiwa inawezekana
kabisa tusiweze kustahilimi tukamuasi Mungu mara moja.
Yohana 6: 26
Kwenye harusi za siku hizi, watu hawaendi kanisani
kushuhudia ndoa halisi, ila wanakwenda ukumbini kwenye sherehe ambapo hakika
wanajua watakula na kunywa hata miili yao itosheke. Pia kwenye ugonjwa au shida
ni wachache wanaoonekana kuliko kwenye sherehe na furaha.
Ayubu hakumkataa Mungu, wala kutenda kosa kwa namna yoyote
ile pale alipopatwa na majanga ya kuibiwa mali, watoto wake kufa na yeye
mwenyewe kupata majipu mabaya sana, lakini alisimama imara akimtumainia Mungu.
Mungu anatupenda wakati wote, tunapokuwanacho hata tusipokuwanacho kwani Yeye ndiye
anayetupatia vyote maana ni mali yake Yeye.
Nataka
nikupe moyo ndugu yangu, zaidi sana unapukuwa katika wakati mzuri usistarehe na
kujisahau ila mtafute Mungu kwa bidii sana, kwani maombi yako yatafanyika akiba
katika siku zijazo upitapo katika majaribu, na hakika Mungu atakuvusha na
kukuokoa akikusimamisha tena, cha msingi ni kutokata tamaa katika mabaya yote.
Zaburi
30:5b