Kwako nitajificha.
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.
Kwa kazi zote pia
Sitimizi sheria.
Nijapofanya bidii,
Nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa;
Ndiwe wa kuokoa.
Naja msalabani;
Nili tupu, nivike;
Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja,
Nioshe nisijafa.
Na kwenda kaburini;
Nipaapo mbinguni,
Na kukwona enzini;
Roho yangu na iwe
Rahani mwako wewe.